Tulikuwa Na Mahusiano Mimi Na Dada Pasipo Kujijua



Nilikulia kwa bibi mzaa baba, na mama yangu sikuwahi kumuona hadi namaliza darasa la saba.Kwa bahati nzuri nilifanikiwa kujiunga na shule moja ya sekondari iliyopo mkoani mbeya wilaya ya mbozi.

Nikiwa kidato cha pili kabla hatujafanya mtihani wa taifa mwaka 2010,alihamia dada mmoja nilimfaham kwa majina Mawili tu kama ilivyokuwa kwangu pia nilikuwa nayo mawili,tofauti na ilivyokuwa kwa wenzetu,yaani kwa mfano, John Husein na si matatu.

Dada huyu aliletwa na mama mmoja ambaye mimii sikumuona , lakini walio muona walidai anafanana kwa kiasi flani namim na kitu hicho kilimfanya yule dada anipende ghafla baada yakuambiwa mama yake anafanana na mimi.

Tulishirikiana kwa kila kitu kusoma,kula, hadi ikafika hatua walimu walituita mara kadhaa kutuhoji!, lakini walibaini hakuna mahusiano mabaya kati yetu,isitoshe mimi nilikuwa nakaumbo kadogo ukilinganisha na yule dada.

Tulipofika kidato cha 3 mwaka 2011, mama yake alikuja kumtembelea huyu rafiki yangu na akawa ameomba kuonana na mimi, lakini walimu walimkatalia kwani haikuwa rahisi sana mtu asiekuwa mzazi kuonana na mwanafunzi mwingine, hivyo yule mama aliishia kusikia tu yule dada akinisifia kuwa mim nirafiki yake mwema sana na kuwa tunafanana sana mama yake(yeye) lakini hakujua mtoto mwenyewe nikoje.

Urafiki wetu ulizidi kushamiri na kunawiri kila ilipoitwa siku,tena wengine walituonea wivu tulivyokuwa tunapendana nakusaidiana huyu dada.

Ili tuelewane vizuri nitamtaja huyu dada kwa herufi moja ya kwanza ya jina lake yaani Z.

Nakumbuka siku hio tulitakiwa kesho yake kwenda study tour huko Ndolezi-mbozi kuangalia kimondo, kwani ilikuwa kawaida kwa wanafunzi wa kidato cha 4 kwenda huko kila mwaka katika shule yetu.Z aliniambia kuna kitu ataniambia tukiwa tumefika kule au tukiwa njiani kama tu mazingira yatarusu.Nilikuwa nahamu sana kama mgonjwa atamanivyo kupona,au mkosaji atamanivyo msamaha kujua kitu anachotaka kunambia,hamu yenyewe ilizidi hasa pale aliponambia kama nitamkubalia ombi lake basi atanipa zawadi.

Lakini kwa bahati mbaya au nzuri kabla hatujaenda kwenye hio tour mke wa mwalimu wetu wa darasa aliuugua na kufa usiku uleule,alugua malaria akiwa mjamzito.Hali iliyopelekea safar yetu kuahirishwa na kuwa tungeenda siku nyingine.

Lakini kwa kuwa bado tulitakiwa kwenda msibani mbali kidogo na shule kwa usafiri wa roli,mim na Z tulibahatika kukaa karibu, tukiwa kwenye roli Z alinisogelea zaidi na kunambia B,kwani alizoea kuniita hivyo ikiwa pia ni herufi ya kwanza ya jina langu..hivi unaonaje tupange mipango ya maisha ya hapo baadae?,
Z aliniuliza.Mimi nilimuangalia tu kisha nikacheka kidogo na nikamuuliza kwani unaogopa kufa?, Nikiamini amefikiria mengi sana kuhusu kifo cha Mama M,kwani jioni yake Z alikuwa ameenda kununua maandazi kwa mama M hivyo nilidhani labda hilo linasumbua,na kwakuwa Mama M,alikuwa amefariki ghafla akiwa kwenye harakati za kujifungua,nilihofu kuwa huenda ndio shaka yake.

Z akasema hapana B , pamoja na kuwa leo tumekutwa tatizo la msiba na safari yetu kuahirishwa, mim bado nitakuwa sijaitendea haki nafsi yangu kwa kutokukuambia nilichokuwa nimekipanga kukisema, ukizingatia siku ya leo nilipanga siku nyingi sana kama ningetekeleza adhima yangu,alisema Z huku akitiririsha machozi ya upendo toka kwenye jicho lake la kushoto.

Ilikuwa ni mwezi wa nane na kipindi hicho kwa kule mbozi kunakuwa jua na vumbi sana.Hata hivi kwakuwa tulikuwa kweye roli haikuwa rahisi sana wanafunzi wenzetu na watu wengine walikuwemo kwenye roli kusikia maongezi yetu, kwani watu walikuwa wanapiga makelele kama tu ilivyokuwa kawaida kwa wanafunzi,na kwakuwa barabara ilikuwa ya vumbi tulitumia nafasi hio kujifunika kitenge cha Z alichokuwa amekipulizia marashi ya aina yake na hata pamoja na Vumbi sisi tulijihisi tupo ufukweni tukifaidi hewa murua na safi.Tulifanya hivyo ili sale zetu zisichafuke sana kwani ilikuwa pia tabia yetu kuonekana wasafi muda wote.

Wakati Z anaeongea huku anabubujikwa na machozi ilihali mimi nikiwa sipendi kumuona akilia,
nilimkatisha kuwa tutajadiliana mara baada ya kumaliza mazishi,alinielewa na kisha tukaendelea na safari.

Tulisafiri na safari yetu ilituchukua takribani masaa matatu hivi tukawa tumefika kijiji kimoja kinachoitwa Ipapa.Huko ndiko kulikuwa kwao Marehem mama M,na taratibu zote zilifanyika akazikwa yule mama yetu kipenzi!,ikumbukwe kuwa shuleni tulikuwa tunaishi na baadhi ya walimu kama tu ilivyokuwa kawaida kwa shule za binafsi,hivyo Mama huyu alipendwa sana na wanafunzi wakati wa uhai wake.

Labda itakuwa Alipendwa kwa sababu alikuwa anatuuzia maandazi kwa uficho mara tukitoka prep.

Tulimpenda sana kwa sababu hio ya kuwa alikuwa ni mama pekee aliekuwa akitupikia maandazi na kutuuzia kwa siri,kwani mkuu wa shule na walimu wote walikwa hawarusu vitu kama hivyo kuletwa shule.


Nakumbuka tulipofika shule toka Kule Ipapa, Z alinambia alikuwa hajisikii kusoma siku ile kwa sababu ya uchovu lakini pia kwa sababu ya safari kuahirishwa lakini mbaya zaidi kwa sababu hajatimiza adhima yake ya kunambia alichotaka kunambia.

Mimi nilimwambia aje prep.(kusoma) ili japo tuzuge.Z alifanya hivyo na kisha akaja na tukakaa nyuma kabisa ya darasa tofaut na siku za nyuma.
Alitumia nafasi hio kuniambia kuwa ananipenda na anahisi kwakuwa si muda tunatakiwa kufanya mtihani wa kidato cha 4 basi tukiwa tumerudi majumabani kwetu kila mmoja wetu ajue kuwa anamwenzake.

Hata sikusita kumkubalia kwani nilitamani sana kama ningepata nafasi hio ya kuwa na mtoto wa Kinyiha(kabila dogo sana wilayani mbozi),mweusi,mrefu,mwembamba kiasi na mwenye kiuno kilichojigawa kama kiuno cha nyigu!.Nilijihisi nimepata tiba ya ugonjwa ambao haukupata tiba mda mrefu,japo nilikuwa sijawahi kuwa na mpenzi katika maisha yangu,kwa bahati mbaya nilikuwa kijana mpole,mwenye adabu na heshima na nilikuwa naogopa kama binadamu aogopavyo kufa kumwambiavbinti ati "nakupenda"! 

Ukiachilia mbali malezi ya bibi yangu,alieniambia nisije nikajihusisha na mambo ya mapenzi shuleni,hivyo sikutaka kumsaliti bibi yangu kipenzi lakini pia Z alichangia sana mim kuwa hivyo kwani nilikuwa siwezi kuongea na binti yoyote zaidi yake yeye.

Tarehe 27/9/2012 ilikuwa siku mhimu sana kwetu na hivyo kila mmoja mzazi wake alitakiwa kuja kwenye mahafali ya kidato cha nne.Baba yangu alikuja na mama yake Z akawa amekuja pia sherehe zilifaana saana.

Mimi na Z tulionekana vijana wa ajabu sana kwani wakati wa zawadi aidha nilienda mim au Z kila walipo ita majina ya wanafunzi walio fanya vizuri kwenye mitihani ya utamilifu (mock exams) iliyokuwa imefanyika mwezi mmoja nyuma ,yaani kama somo fulani hakuongoza Z basi niliongoza mimi,Hali ambayo iliufanya Ukumbi ujae vifijo na na miruzi toka kwa wenzetu na wengine walisikika wakisema hawa watoto watakuwa mapacha wasio fanana!.

Lakini cha ajabu sana ambacho kilinifanya nishangae, baba yangu Mzee F alionekana kuwa na furaha sana na hata tulipofika kwenye kisherehe kidogo cha kifamilia alienda kwenye chumba cha akina Z.

Mimi nilihisi kuwa watakuwa wamehisi kuwa sisi watoto wao tunapendana hivyo wanatarajia kuwa tutaoana baada ya kumaliza masomo yetu, kama tuliyokuwa tumekubaliana siku chache nyuma mimi na Z.
Jioni yake kabla ya wazaz kutawanyika Mama Z alinipa Zawadi ya suti na kunisistiza kusoma,lakini kitu ambacho kilinishangaza sana nilihisi maongenzi fulani yaliendelea kati ya mama Z baba yangu,sikupata nafasi ya kuwasikilza vizuri.

Wakati mlinzi anawatangazia watu wasio kuwa wanafunzi waondoke eneo la shule na kuwa muda umeisha, kwa mbali nilimwona na kumusikia Baba yangu sakisema, Hapana Mama Z tusiawambie leo utawathiri watoto kisaikolojia na hata kusababisha washindwe kwenye mitihani yao iliyopo mbele yao hivi karbuni.

Nilikuwa nimesha fika karbu yao na kuwapa begi walilokuwa wamebebea zawadi zetu baada ya kuzipeleka bwenini,hivyo mama Z alibinya jicho lake la kulia kama ishara ya kumfanya baba yangu ajue kuna mtu asietakiwa kusikia maongezi yao kafika!.hali iliyoniachia maswali mengi sana.
Hivi hawa watu wamefahamiana leo au siku nyingi?,je wanajua kama sisi watoto roho na nyoyo zetu zimesha nasana kwenye mtego wa panya?,Na kama wao pia wakaanza kuhusiana si itakuja kuwa balaa tukija kuwaambia tuanataka kuoana?.

Maswali hayo yalinizunguka kichwani huku nikiwa nafunga begi la baba kwenye pikipiki aina ya T better aliyokuwa amekuja nayo kama usafiri siku ile.
B,B, B...Mara tatu nakuita hunisikii kweli,inamaana unatumia akili nyingi sana kufunga begi hapo jamani acha makusudi hayo bwana!,aliskika Z huku akiinamisha kichwa kunitizama nilivyokuwa nafunga begi kwenye pikipki na kunishika kiunoni,nilistuka na kutoa sauti iliomstua Mama Z pia,kwani nilikuwa nawaza vitu vingi sana kwa wakati ule na hata sikutambua uwepo wa Z.
Mama Z alishika kichwa na kisha kumwambia Z acha utani wa kihivyo kwa kaka yako nawewe!...,eee mama nawewe hili ndio jembe langu bila yeye mimi si Z tena!,alijibu Z.

wakati huo Baba alikiwa anapiga kiki mara kadhaa ili aanze kuondoka, na mama Z anaingia kwenye gari lake aina ya lav 4 New model huku Z akimukumbatia mama yake kama ishara ya kuagana.

lakini hali ilibadilika sana kwani kwa vitendo vilivyofanyika pale kwa mda mfupi, viliwafanya Baba yangu na Mama Z kuwa na hofu na ukarbu wetu.Kitendo kilichomfanya mama Z amkonyeze baba kama.ishara ya kuwa asiende haraka waonane mbele kidogo,nje ya eneo la shule.

Sisi tulianza kurudi huku tumeshikana mikono,mara honi ya gari ilisikika pii piipii...mara tatu,tukaangalia nyuma,kumbe alikuwa mama Z akiwa anamuita Z kwa kuashiria kushitushwa kidogo na tendo la kushikana mikono kwa namna ile,Z akawa anarudi ili amsikilize.


Mwanagu, huyu ni sawa na kaka yako kabisa!,si vizuri sana kumshika namna ile, hauoni inaashiria kuwa hamna tabia nzuri?.Mama Z alihoji huku akionekana mwenye kutafakari sana namna na jinsi ya kumfanya mtoto wake apate ujumbe wa yeye kutopenda hali ile.
Huku ameweka shingo yake upande wa kushoto nakuinama chini akisugua aridhi kwa kidole gumba cha mguu wa kulia kilichojificha ndani ya kiatu ,Z hakujibu chochote.Mama Z aliwasha gari na kisha kuondoka.

Vipi mbona umekawia sana mama Z?,Alihoji Mzee F aliekuwa ameegesha pikipiki yake chini ya mti akimsubiri Mama Z ili waangalie namna ya kuwafanya watoto wao wajue siri nzito iliyojificha kati yao.

Bila shaka umeona kuwa huu sio mda wa kulaaumiana tena na tofauti zetu tuziweke pembeni ili kunusuru watoto hawa wasije wakaanza mahisiano yasiyo faa,alieendeleza kusema hivyo Mzee F.Mama Z akikumbuashia enzi zake alivyokuwa mwanamke mtiifu dhidi ya mtaraka wake alisema ni kweli mtupu Baba Z,panga lini turudi tena.

Nivema tukaja baada tu ya wao kumaliza mitihani au una mapendekezo mengine?.Mama huyu alieonekana kujutia kumuacha mume aliempenda kwa dhati,lakini alimuacha baada ya kurubuniwa na mfanya biashara mmoja wa kahawa hata kumfanya apewe taraka miaka 20 iliyopita.alijibu kwa upole "haina shida baba Z".

Ulikuwa usiku mrua kwa Mimi na Mpenzi wangu wa kipekee,kwani alivaa tofauti kabisa na siku nyingine,alivaa gauni jekundu,fupi lilichora umbile lake na kuangaza kwa mtu alie msogolea iliyofanya watu wamuite kwa sauti "mrembo wa kinyarwanda huyo!" Waliita hivyo kutokana na umbo lake lilokuwa linamfanya awe gumzo hata kwa mabinti wenzake.Moyo wangu ulienda mbio kwani alinivutia sana.

Mziki ulianza kuzinduliwa na mwalimu wetu wa michezo,mr Sengo alituruhusu tufurahi lakini nidhamu itawale ukumbi.

Tulijikuta tumeshikana viuno na kucheza kwa ustadi mkubwa sana, hasa baada ya Dj kucheza wimbo,"where does my heart beat now?",wa Mwanadada Celine Dion,na nilijikuta nazidi kuchanganyikiwa ulipopigwa "The power of love" kabla hajaanza kucheza mbongo flavour na hasa wimbo wa Vaileti wa matonya uliokuwa kipenzi sana kwa wanafunzi wa shule kwa wakati ule.

Dj alikuwa kama anatii mahitaji ya myoyo yetu kucheza nyimbo zile.hakika tuliburudika kwa namna yakipekee usiku ule.Ukizingatia Celine alikuwa kipenzi sana kwetu.

Juma la mitihani lilikaribia na mitihani ikafanyika,ilidumu kwa takribani majuma mawili hivi siku tunamaliza, tuliambiwa tusiondoke kwani Tungefuatwa siku ileile.Hivyo baada ya kumaliza kukabidhi kila kilichokuwa cha shule,tuliruhusiwa kwenda kuzunguka mjini (nje kidogo ya shule).


Kwakuwa walimu walikuwa hawajawahi kuwa na mashaka juu ya ukaribu wetu,hakika hawakuwiwa ugumu kuturuhusu kwenda mjini pamoja.Walisisitiza kuwa tuwahi kurudi kwani mida ya saa kumi jioni kuna mtu angetufuata.

Masikini Mama Z!,Akiwa kwenye harakati za kumpitia Baba F na kisha waje shule,gari lake liligongana uso kwa uso na gari moja ya mizigo aina ya fuso,ajari iliyopelekea mama Z kuvunjika mguu wake wa kulia, lakini pia alipoteza fahamu na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Kuwepo kwetu mjini bila shughuli maalumu ndiko, kunakonifanya leo nisimulie kisa hiki kinacho uumiza moyo wangu kila ninapofikilia kuhusu mapenzi.

Nakumbuka mim ndie niliemshawishi Z kuwa tuende sehemu ya faragha japo kwa mara ya kwanza,lakini pia kama namna ya kuagana.Hili halikuwa tatizo kwa Z shida ilikuwa twende wapi na ikiwezekana iwe haraka ili tusichelewe shule.

Tulijikuta tupo kwenye nyumba ya wageni,na kila mmoja anashangaa kilichotokea!.Hii haikuwa hali ya kutufanya tushangae sana bali wakati tunaingia ndani,pamoja na kuwa kulikuwa kelele za muziki lakini nilimfanya Z alie kwa kile alichodai kama ntakuja kumtenda basi atajiua au hata kuniua mimi!.

Nilijihisi kuwa mwanaume sasa ukizingatia ndio kwanza ilikuwa mara yangu ya kwanza,kukutana na binti na hasa binti mzuri wa aina yake,hakika nilijihisi mwenye bahati ya kipekee kuwa nae.Na hilo alilijua japo nae alisema hivyo hivyo pia kunihusu.

Haikuwezekana tena Mama Z kuja shule wala mzee F.Tulipofika shule tuliambiwa kuna mabadiliko ya taarifa hivyo tulitakiwa kuondoka jioni ileile na si kuja kuchukuliwa tena kama ilivyokuwa awali.

Hakika mapenzi yalizidi kunoga,tulianza safari pamoja kwani tulitakiwa kuondoka na Z alitakiwa kupitiliza hadi Mbeya mjini.Wakati mimi nilitakiwa kushukia Mlowo kilomita kadhaa kutoka shuleni.halikuwa tukio rahisi sana kuachana lakini ilitulazimu.

Ilikuwa jumapili asubuhi,kabla hatujaamuka kwenda shambani na bibi yangu kipenzi,Nilimkuta baba akiwa nje anasubiri tuamke,alionekana ni mtu asiekuwa na raha hata kidogo nilimhoji baba kwanini mbona huna raha hata kidogo?.aliingia ndani huku akiuliza bibi yako yuko wapi?.nilimwambia yupo ndani.

Alimuita bibi kisha wakaongea kwa muda maongezi yaliyo chukuwa kama nusu saa hivi,nilikuwa nimesimama nasubiri twende shamba na bibi.kabla sijawaambia kama ningetangulia shamba ili bibi anikute huko.bibi aliniambia nirudishe majembe ndani tutaenda siku nyingine,lakini pia alionekana kama kuna taarifa mbaya kazipata kwani alionekana kubadilika ghafla.

Wakati narudisha jembe ndani nilimuona baba akiongea na simu akimuomba mtu fulani ambae mimi sikuweza kumjua lakini walionekana wakiongea maongezi yao yaliyo husiana na mazishi ya mtu ambae mimi sikujua ni nani,sikiliza bwana Simba,huyu mama akazikwe kwao,na mtoto wangu nitamchukuwa,nitawalea wote mbona mwenzake nimemulea na sasa anaendelea vema.Alisikika akiongea baba F huku akionekana hana mahusiano mazuri na mtu wa upande wa pili ambae mimi sikumjua.

Huku naendelea kuhamaki, kumuona baba yangu akibishana kwa mara ya kwanza,bibi aliniita kuwa nijiandae ili twende msibani.Nilimhoji nani kafa aliniambia kuwa atanifahamisha hukohuko.Nilianza kujiandaa huku nina maswali mengi sana kichwani.nani kafa,na kwanini nisiambiwe,na sina dungu yoyote wa karibu ambae alikuwa anaumwa hivi karibuni.

Tulianza safari,tulipofika stand kwenye barabara ya lami,baba alituambia tupande gari,yeye atatufuata kwa pikipiki yake,kwani askari wa barabarani walikuwa hawaruhusu kubebana zaidi ya watu wawilikwenye pikipiki.Tuliingia kwenye gari kwenda huko Tukuyu. Tukiwa njiani nilijaribu kumdodosa bibi aniambie nani kafa lakini bibi alijifanya kachanganyikiwa na hata kutoniambia nini kinaendelea.

Mungu wangu kumbe Mama Z,kafa!. Jamani mama huyu alikuwa ananipenda kama mwanae wa kuzaa leo kafa!,nilijikuta machozi hayaishi kumiminika,kila nilichotaka kutamka kilibanwa na kwikwi lilitokana na majonzi yaliyokuwa ndani ya moyo wangu.Nilijihisi mtu mwenye huzuni ukizingatiq nilikuwa sjiawaho kufaidi matunda ya kuishi na mama, nilipomuona Z ameshikwa na akina mama wawili akiwa hana nguvu hata kidogo na mda huo tunafika ndio mda maiti alikuwa anapelekwa kaburini tatayari kwa mazishi.

Hakika moyo wangu ulisononeka sana,nilijihisi mkosaji asiyestahili msamaha,nilitamani kaburi jingine lichimbwe niingie na nifukwe sio tu kwa sababu ya kumpoteza mama yangu pekee ,bali ni baada ya kujua ukweli kuhusu mimi na Z.

Marehemu alizaliwa mwaka 1978,hapahapa Tukuyu,na alisoma shule ya msingi Mpuguso,aliolewa kwa mara ya kwanza na bwana Fracksoni G mwashilindi huko Mbozi,Alibahatika kuzaa nae watoto wawili tu, ambao ni Zena F.mwashilindi na wa pili Bahati F mwashilindi.Lakini baada ya hapo aliolewa kwa Bwana Simba ambako hakubahatika kupata mtoto hata mmoja.Na hadi anapatwa na mauti alikuwa ni mke halali wa Bwana simba.mauti haya yametokana na ajari ya gari aliyoipta akiwa safarini kwenda wilayani Mbozi.Mungu ailaze roho ya marehemu pema pepononi amina!.Alimaliza hivyo msomaji wa historia fupi ya marehemu.

Sijui kama Zena aliskia kwa umakini historia ya marehemu mama yetu.Niliiona siku ile kuwa nyeusi iliyokuwa imefunikwa na wingu la ajabu!,kwani ilijaa taarifa mbaya kwangu ambazo kiuharisia zilifanya uwezo wangu wa kutafakari mambo kuzidiwa.sikujua ningeanzaje kumwambia baba yangu kuwa wamechelewa sana kutuambia sisi ni ndungu tena ndugu wa damu, mbaya zaidi watoto pekee wa familia ya Mzee mwashilindi.Ee Mungu nisamehe mimi....

Hakika sikuona umuhimu wa kuendelea kuwepo mahala pale niliondoka kwenda mahala kusiko julikana hadi leo naandika simulizi hii sijui baba yangu yuko wapi,wala sijui Zena aliko.Dada yangu pekee ambae kwa uzembe wa wazazi wetu tumejikuta tunahusiana kimapenzi kwa sababu hatukujuana. Ningemuona nisingetamani kuonana nae kwani ningekosa cha kumwambia.Inaniuma sana lakini ndio hivyo majuto ni mjukuu.

Tunakuomba follow hii blog katika sehemu ya followers ili upate taarifa pindi tu zitakapo kuwepo
https://alvinhabari.blogspot.com

Pia share na wengine 

No comments

Theme images by konradlew. Powered by Blogger.