Muonekano mpya Wa Santiago bernabeu 2022

KWANINI REAL MADRID WAMEHAMA SANTIAGO BERNABEU?!.
.
Kama umegundua siku za hivi karibuni tangu baada ya Corona michezo ya Real Madrid ya nyumbani imekua ikichezwa katika uwanja wa Estadio Alfredo Di Stefano na sio Santiago Bernabeu kama ilivyozoeleka.
.
Kumeelezwa sababu nyingi na wengi wakiamini kuzuiwa mashabiki kuingia uwanja kuliwafanya Madrid kuacha kuutumia Bernabeu kuepuka gharama za matengenezo kila baada ya mechi,na wakaona labda kutumia Di Stefano itawasaidia katika gharama.
.
Lakini ukweli ni kwamba Bernabeu upo katika matengenezo na maboresho makubwa ambayo yatachukua muda,taarifa zinasema kuna uwezekano hata msimu ujao wa ligi Madrid wakakipiga Di Stefano kwani matengenezo ya Bernabeu yanaweza kuisha mwaka 2022.
.
Di Stefano umekua ukitumika kwa ajili ya timu ya vijana ya Real Madrid(Castilla) na una uwezo wa kuingia mashabiki 6000 tu jambo ambalo sio tatizo kwa Madrid katika kipindi hiki.
.
Matengenezo mapya ya Real Madrid yanaweza kugharimu kiasi cha €796.5 million na picha hapo juu ni muonekano wa namna Bernabeu itakavyoonekana baada ya matengenezo.
.

No comments

Theme images by konradlew. Powered by Blogger.