Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi 01

Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi 
Sehemu ya kwanza


Uhamisho wangu wa kikazi kwenda
Tanga
ulikuja kama adhabu kutokana na
ukiukaji wangu wa maadili ya jeshi la polisi
nikiwa
muajiriwa wa jeshi hilo.
Nilijiunga na jeshi la polisi miaka mitano
iliyopita mara tu baada ya kuhitimu
kidato
cha sita huko Kagera ninakotoka.
Nilipomaliza mafunzo yangu ya upolisi
huko Moshi nilipangiwa kuanza kazi jijini
Dar. Mimi na wenzangu kumi na wanane
tuliuopangiwa kwenda Dar tulifurahi sana
na kujiona tulikuwa na bahati
kuchaguliwa kwenda Dar kwani wenzetu
wengi
walikuwa wakililia kupangiwa kazi katika
jiji
hilo.
Kituo changu cha kazi cha kwanza jijini
Dar, kilikuwa kituo cha polisi cha Ilala. Pale
nilipelekwa peke yangu. Wenzangu
walitawanywa katika vituo vingine
vilivyotapakaa sehemu mbalimbali za jiji.
Katika kipindi cha miaka minne ya
mwanzo nilifanya kazi kwa bidii na uaminifu
mkubwa. Kwa vile kazi yenyewe
niliipenda
niliifanya kwa kujituma na kwa weledi.
Mara
kadhaa nilisifiwa na wakuu wangu na
kutolewa mfano kwa wengine.
Siku moja mimi na polisi mwenzangu
tulitakiwa kusindikiza gari lililochukua
mishahara ya wafanyakazi wa kiwanda
cha
bia kutoka benki moja iliyokuwa barabara
ya Samora na kuipeleka kiwandani hapo.
Ilikuwa ni kawaida kila ifikapo mwisho wa
mwezi, mashirika ya serikali huomba
askari
kwa ajili ya kusindikiza mishahara ya
wafanyakazi kutoka benki. Ilikuwa ni nafasi
nzuri ambayo polisi
wadowadogo tulikuwa tunaigombania
kwa
sababu ilikuwa na posho kidogo. Siku
hiyo
nikapata bahati hiyo mimi na mwenzangu.
Tulipakiwa na gari ya kiwanda hicho
lililotufuata kituoni. Mimi na mwenzangu
kila
mmoja alikuwa na bunduki yake aina ya
SMG iliyokuwa na risasi tisini.
Tulipofika benki tulisubiri nje ya gari.
Sanduku la pesa lilipotolewa tulishika
bunduki zetu vizuri na kuangaza macho
kila
upande kuhakikisha usalama wa pesa hizo.
Sanduku hilo lilipopakiwa kwenye gari na
sisi tulijipakia. Gari likaondoka. Tulifika
kiwandani salama. Gari likasimama
kusubiri
kufunguliwa geti ili tuingie ndani ya eneo la
kiwanda.
Wakati askari anakwenda kutufungulia
geti,
gari moja likasimama ghafla ubavuni
mwa gari tulilokuwemo. Ndani ya gari hilo
mlikuwa na watu watano akiwemo
dereva.
Mara tu baada ya gari hilo kusimama
watu
wawili miongoni mwa watano
waliokuwemo ndani, walipenyeza mitutu
ya
bunduki kwenye madirisha na kuanza
kutushambulia kwa risasi za mfululizo.
Mimi na polisi mwenzangu tuliinama
chini. Risasi zilivunja vioo vya gari vya
ubavuni,
zikawa zinapita juu ya vichwa vyetu.
Maafisa
watatu wa kiwanda hicho waliokuwemo
ndani ya hilo gari walipoona
tunashambuliwa walifungua mlango wa
gari wa upande wa pili na kukimbia.
Baada ya maafisa hao kukimbia na
kuliacha
sanduku la pesa ndani ya gari, tulisikia
kimya halafu tukasikia hatua za watu
wakija mbio. Nikahisi walikuwa ni
majambazi
waliokuwa wakitushambulia , sasa
wanalifuata lile sanduku la pesa baada
ya
wenyewe kukimbia.
Hapo hapo nikatoa mdomo wa bunduki
kwenye dirisha na kuanza kufyatua risasi
mwenyewe nikiwa nimeinama.
Mwenzangu
naye alifyatua risasi lakini alikuwa
ameinua
kichwa chake, akapigwa risasi ya kichwa na
kufa pale pale.
Nilipomuona mwenzangu ameuawa
niliacha
kufyatua risasi nikatulia kimya. Nilikuwa
nimeinama chini ya dirisha ili watu hao
wasinione.
Majambazi hao walipoona hatujibu
mapigo
walijua kuwa wameshatuua. Tamaa ya
pesa
ikawafanya waharakishe kufungua mlango
wa gari wakiamini kuwa wameshazipata
pesa hizo.
Vile wanafungua tu mlango huo
walikutana
na mtutu wa bunduki. Niliwafyatulia risasi
majambazi wawili bila wao kutegemea
wakaanguka kando ya mlango wa gari.
Majambazi wengine wawili waliokuwa
nyuma yao walipoona wenzao
wameshambuliwa na risasi zilikuwa
zinaendelea kurindima waligeuka nyuma ili
wakimbie lakini hawakulifikia hata gari
lao
nikawalaza chini wote.
Jambazi mmoja aliyekuwa amebaki
kwenye gari kwenye siti ya dereva aliliondoa
gari
hilo kwa kasi kusalimisha maisha yake.
Sikutakakumkosa yule jambazi,
nikapituka
kwenye siti ya dereva amabayo ilikuwa
tupu. Gari hilo lilikuwa kwenye moto, nikatia
gea
na kulifukuza lile gari.
Wakati naliondoa gari hilo niliwakanyaga
majambazi wawili waliokuwa wamelala
chini na kuwatoa matumbo! Gari hilo
halikufika mbali nikaliingia
ubavuni.
Nililibana na kulibamiza
pembeni mwa barabara kisha nikalichota
na
kulipindua kichwa chini miguu juu, likawa
kama mende aliyekufa huku tairi zake
zikiendelea kuzunguka zenyewe.
Kulikuwa na gari la polisi lililokuwa
kwenye
doria. Polisi hao walipoona tukio hilo
walisimamisha gari. 


Na mimi nikashukuru
kwa kuona nimepata msaada. Nilishuka
kwenye gari nikaona gari jingine la
kiwanda
cha bia likisimama nyuma ya gari la
polisi.
Bila shaka gari hilo lilikuwa likitufuata
nyuma.
Polisi wanne walishuka kutoka gari la
polisi
na maafisa wanne walishuka kutoka gari
la
kiwanda cha bia, watatu walikuwa ni wale
tuliokwenda nao bemki. Nilijua kwamba
walikuwa wakifuatilia pesa zao.
Nikafungua
mlango wa gari nikalitoa lile sanduku la
pesa na kuwakabidhi. 

Itaendelea tena kesho....
Ili usipitwe na simulizi hii kali Hakikisha unaenda sehemu ya followers  una follow hii blog ✨


No comments

Theme images by konradlew. Powered by Blogger.