Kim Jong-Un Arejea tena


Kim Jong-un ameonekana hadharani kwa mara ya kwanzabaada ya siku 20, vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimesema.
Shirika la habari la KCNA limeripoti kuwa kiongozi huyo wa Korea Kaskanzini alikata utepe katika ufunguzi wa kiwanda cha mbolea. i
Liliongeza kuwa watu katika kiwanda hicho '' walimshangilia kwa furaha kubwa" alipojitokeza siku ya Ijumaa.
Taarifa za kuonekana kwake-mara ya kwanza tangu alipoonekana katika tukio kwenye vyombo vya habari vya taifa hilo tarehe 12 Aprili- zinakuja huku kukiwa na tetesi kote duniani kuhusu afya yake.
Taarifa za hivi punde kutokavyombo vya habari vya taifa la Korea Kaskazini hazikuweza kuthibitishwa.
Vyombo vya habari baadae vilitangaza picha ambazo zilionyesha Bwana Kim akikata utepe nje ya kiwanda.
Alipoulizwa kuhusu taariofa za kuonekana kwa Kim, rais wa Marekanai Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa asingetaka bado kuzungumzia lolote juu ya taarifa hizo.
Je rip[oti ya vyombo vya habari vya taifa inasemaje?
Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa- Korean Central News Agency (KCNA), Bwana Kim aliambatana na maafisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini, mkiwemo dada yake Kim Yo Jong.
Kiongozi wa Korea Kaskazini akakata utepe katika sherehe iliyofanyika katika kiwanda, katika jimbo la kaskazini mwa nchi la Pyongyang, na watu waliohudhuria tukio hilo " walimshangilia kwa shangwe kubwa ' kiongozi huyo wa ngazi ya juu ambaye anawaamuru watu wote kwa ujumla kutimiza jukumu zuri la mafanikio ", KCNA ilisema
Tunakuomba nenda sehemu ya followers then follow this blog ili uwe wakwanza kupata habari.

Please  share..

No comments

Theme images by konradlew. Powered by Blogger.