Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi sehemu ya 13

Baada ya kumaliza maelezo yake
ambayo yaliwashangaza maafisa
hao, kamanda wa polisi akataka na
mimi nieleze kilichotokea.
“Kwanza ulifikaje katika eneo hilo
na ulikuwa na Sajenti Erick au
ulikuwa peke yako?” akaniuliza.
“Nilikwenda peke yangu” nilimjibu.
“Kufuata nini?”
Niliona kama nitauma uma
maneno nitajikuta nikiwekwa
ndani, jambo la msingi ni kueleza
ukweli wote.
“Kuna msichana niliwasiliana naye
kwenye simu akataka nimfuate
katika eneo hilo”
“Ni nani?”
“Wakati tunawasiliana nilikuwa
simjui lakini baadaye niligundua
alikuwa ni yule msichana ambaye
mama yake tulimshitaki kwa
kukutwa na kete za madawa ya
kulevya na mama mwenyewe
akafia mahabusi”
“Umesema wakati mnawasiliana
ulikuwa humjui,?”
“Nilikuwa simjui”
“Uliwasiliana vipi na mtu ambaye
ulikuwa humjui?”
SASA ENDELEA.
Swali hilo lilinifanya nieleze ukweli
wa tukio zima la kuwasiliana na
Maimuna. Nilianzia pale alipokosea
namba akanitumia meseji.
Kamanda baada ya kunisikiliza
aliniuliza.
“Kwa hiyo ulipokuwa unakwenda
kuonana naye ulikuwa na
madhumuni gani?”
“Nilikuwa nataka tuwe marafiki, si
unajua afande mimi sina mke”
Nilipojibu hivyo Kamanda wa polisi
akamtazama Afisa upelelezi kisha
akaendelea kunihoji.
“Enhe, ulipofika hapo mahali
alipokwambia mkutane nini
kilitokea”
“Nilipofika pale sikumkuta,
nikampigia simu kumuuliza yuko
wapi”
“Ndiyo”
“Akanijibu kwamba yuko nyumbani
kwao hivyo nimfuate na
akanielekeza njia ya kufika
nyumbani kwao”
“Ukaenda?”
“Nikaenda. Njia yenyewe ni ya
kwenye mapori. Mahali kwenyewe
kuna nyumba moja moja na kuko
giza”
“Ulipofika?”
“Nilikutana naye njiani.
Akanipeleka kwenye hiyo nyumba.
Tuliingia ndani akanikaribisha
ukumbini halafu yeye aliondoka
akaniambia nimsubiri. Lakini kuna
kitu kimoja nataka kueleza”
“Eleza”
“Yule msichana nilimgundua kuwa
ni yule ambaye mama yake
alishitakiwa kwa kukutwa na
madawa ya kulevya hivi karibuni
akafia mahabusi. Nadhani
unakumbuka afande”
“Nakumbuka na niliambiwa
alikuwa na binti yake ambaye
aliwatoroka” Kamanda
alimwambia.
“Basi huyo binti ndiye huyo
msichana mwenyewe”
“Kwa hiyo hakushituka kukuona”
“Hakushituka”
“Na wewe hukumuuliza kitu?”
“Wakati kumbukumbu zinanijia
kujua ni yeye alikuwa
ameshaondoka na kuniacha peke
yangu pale ukumbini ambako
aliniambia nimsubiri”
“Alikwambia anakwenda wapi?”
“Hakuniambia. Basi pale pale
nilipitiwa na usingizi wa ghafla.
Nilipozinduka ilikuwa saa tisa
usiku. Yule msichana sikumuona…”
nikaendelea kueleza kilichotokea
baada ya hapo.
Kile kisa kiliwafanya maafisa hao
wa polisi watazamane kwa
mshangao.
“Una maana yule mwanamke
aliyekufa ulimkuta akiwa mzima
akichimba kaburi?” Afisa upelelezi
ndiye aliyeniuliza.
“Ndiyo. Mimi nilishangaa sana
kumuona” nikamjibu.
“Umetuambia kwamba watu hao ni
majini?” Kamanda akauliza.
“Ni majini. Hata wenzangu
waliokuja wameona kuwa ni
majini”
“Hivi majini ni imani tu au ni
viumbe kweli?”
“Kwa tukio hili mimi nimethibitisha
kwamba majini si imani, wapo!”
“Kwa hiyo majini ndio
wamemchinja Erick?’
“Ndio. Nafikiri ni kwa kisasi cha ile
kesi kwa sababu yeye na mimi ndio
tuliomkamata yule mwanamke”
“Kwa hiyo walikuwa wanataka
kukuchinja na wewe?”
“Ndiyo”
“Kwa vile kuna tukio la mauaji ya
polisi na kiserikali hatuamini
kuwepo majini, tutawachukulia
kuwa hao ni watu na inabidi tukio
zima lithibitishwe” Kamanda wa
polisi akaniambia kisha
akamtazama Afisa upelelezi.
“Itabidi tufike katika eneo hilo la
tukio, tupige picha pamoja na
kuchukua maelezo kwa watu wa
karibu na eneo hilo” Afisa upelelezi
akamwambia kamanda.
“Sawa, itabidi tufike”
“Kuna mtu mmoja tumekuja naye
kwa ajili ya kuandikisha maelezo”
Yule inspekta niliyekuwa naye
akasema.
“Ni nani?” Kamanda akamuuliza.
“Ni mwananchi tu mkazi wa jirani
na mahali palipotokea hilo tukio na
ndiye aliyetupigia simu kutujulisha
kuwa kuna polisi waliolala juu ya
makaburi”
“Hebu mlete hapa”
Inspekta alitoka na baada ya muda
kidogo alirudi akiwa na mtu huyo.
Aliwasalimia wale maafande kwa
uoga.
“Karibu sana” Kamanda
alimwambia ili kumtoa hofu.
“Asante” Mtu huyo alijibu.
“Hebu tueleze ulichokiona huko
Magomeni hadi ukapiga simu
polisi” Kamanda alimwambia.
“Niliona polisi wamelala juu ya
makaburi saa kumi na mbili
asubuhi wakati nakwenda shamba,
ndio nikapiga simu”
“Hao polisi walikuwa wamelalaje?”
Kamanda alimuuliza.
“Walikuwa wamelala usingizi
kabisa na walikuwa na bunduki”
“Hapo mahali ulipowaona palikuwa
na nyumba?”
“Hapana, lile ni eneo la makaburi
tu”
Kamanda wa polisi akanitazama
kabla ya kuuliza tena.
“Tumepata maelezo kwamba wale
askari waliingia kwenye nyumba,
wakazirai na walipozinduka
wakajiona wako juu ya makaburi
na ile nyumba hawakuiona tena”
“Inawezekana. Pale mahali
panatokea miujiza mara kwa mara.
Inasemekana pana majini”
“Wewe uliwahi kuwaona?”
“Mimi sijawahi kuwaona lakini
kuna mtu aliwahi kuona
mwanamke mrefu kama mnazi
amesimama pale usiku”
“Alipomuona nini kilitokea?”
“Yule mtu alikimbia na aliuporudi
tena akiwa na wenzake, huyo
mwanamke hawakumuona tena”
Je nini kitafuatia?e

No comments

Theme images by konradlew. Powered by Blogger.