Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi Sehemu ya 04 hali imebadilika

Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi 04

Ngojeni gari ije twende kituoni ndipo mtakapojua kosa lenu” Erick aliwambia baada ya kuhakikishiwa kuwa gari la polisi linatufuata.
Yule binti alitutoroka pale pale na kupotea. Tukabaki na yule mwanamke.
“Binti yako ametukimbia lakini tutamtafuta” Erick alimwambia yule mwanamke polisi wenzetu walipofika.
Tulimtoa yule mama, tukamwambia afunge mlango wake. Alipofunga mlango wa nyumba yake, funguo zake nilizichukua mimi. Tukampakia kwenye gari la polisi na kwenda naye kituoni.
Wakati mwanamke huyo anahojiwa ndani ya kituo cha polisi, mimi nilitoka nikakodi bodaboda na kurudi nyumbani kwake. Kile kisanduku cha dhahabu kilikuwa kimenitoa roho na Erick alikiacha baada ya kuona ilikuwa mali halali ya yule mwanamke.
Nilifungua mlango wa nyumba yake kwa kutumia zile funguo ambazo nilikuwa nazo mfukoni. Nikaingia ndani. Nilikichukua kile kisanduku cha dhahabu nikakifunga na kitambaa cheupe nilichokikuta mle chumbani kisha nikatoka. Nilipotoka nilikodi teksi ikanipeleka nyumbani kwangu Msambweni ambako kulikuwa na nyumba za polisi.
SASA ENDELEA
Nlipofika nyumbani kwangu, niliingia ndani. Nilikificha kile kisanduku chini ya mvungu wa kitanda changu kisha nikatoka tena na kurudi na ileteksi kituo cha polisi. Zile funguo zanyumba ya yule mwanamke nilizikabidhi kwa Sajenti Erick.
“Nilizisahau mfukoni mwangu” nikamwambia.
Erick alizichukua nakwenda kuzihifadhi kwenye kabati.
Yule mwanamke alikuwa amehojiwa na baadaye kupelekwa rumande. Niliambiwa alikuwa amekanusha kuhusika na zile kete za madawa ya kulevya. Polisi walikuwa katika pilikapilika za kuandaa mashitaka yake ili kesho yake afikishwe mahakamani.
Kusema kweli kukamatwa kwa yule mwanamke hakukuwa halali Sajenti Erick alikuwa ameweka mtego wake apate pesa kwa njia ya kumtisha yule mwanamke lakini mwanamke mwenyewe hakutishika na akawa tayari ashitakiwe kwa kosa la kukutwa na kete za madawa ya kulevya ambazo alizikana.



Siku iliyofuata mwanamke huyo akafikishwa mahakamani. Alisomewa shitaka la kukutwa na kete tatu za madawa ya kulevya, akakana shitaka hilo. Kesi ikaahirishwa nay eye akarudishwa rumande kwa kukosa mdhamini.
Niliusifu sana ujasiri wa Sajenti Erick, kumfungulia kesi mwanamke huyo mzee huku akijua fika kwamba hakuwa na hatia. Zilikuwa ni chuki za kutopata pesa alizotaka kutoka kwa mwanamke huyo.
Na hata kama angebadili mawazo yake, asingeweza kumuachia kwa sababu mtuhumiwa tayari alishafikishwa kituo cha polisi. Mambo hayoyalitakiwa yamalizikie kule kule nyumbani kwa yule mama.
Polisi hawakushughulika tena kumtafuta yule msichana aliyetoroka, wakamng’ang’ani yule mama. Siku ile ambayo alifikishwa mahakamani siku iliyofuata akakutwa ameshakufa.
Maiti yake ilikutwa asubuhi. Ikachukuliwa na kupelekwa hospitali. Sajenti Erick akapata kazi ya kuwatafuta jamaa zake bila mafanikio. Majirani wa yule mama walimwambia Erick kwamba hawawajui jamaa zake. Walikuwa wakimuona yeye na yule binti aliyekuwa naye ambaye alikuwa ametoweka tangu siku alipokamatwa yule mama.
Kesi yake ikafutwa mahakamani. Na baada ya kutojitokeza kwa jamaa yake yeyote, maiti ya mwanamke huyo ikazikwa na manispaa. Tukio lile tukalisahau.
Zikapita siku kadhaa. Kile kisanduku cha dhahabu kilikuwa bado kipo mvunguni mwa kitanda changu. Sikutaka kuziuza haraka haraka zile dhahabu. Nilikuwa nikisubiri muda upite na tukio lisahaulike kabisa.
Siku moja asubuhi wakati natoka nyumbani kwangu naenda kazini simu yangu iliingia meseji. Nilipoisoma ilisema.
“Sitalisahau penzi lako”
Namba iliyotuma meseji hiyo nilikuwa siifahamu. Na mimi nikatuma meseji ya kuuliza.
“Wewe nani?”
Baadaye likaja jibu likisema.
“Samahani, nimekosea namba”
Ile namba nikaizingatia. Jioni nilipotoka kazini nikaipiga. Simu yangu ikapokelewa na msichana.
“We nani?” akaniuliza.
“Mimi ni yule uliyenitumia meseji asubuhi” nikamwambia.
“Ahaa samahani, nilikosea namba”
“Ulikuwa unamtumia mpenzi wako?” nikamuuliza.
“Ndiyo” akanijibu.
“Nilijua kuwa ulikosea namba lakini nilipenda tu kukufahamu, uko wapi?”
“Mimi?”
“Wewe ndiyo”
“Niko Magomeni”
Magomeni ni eneo lilioko pembeni kidogo mwa mji huo. Wakati huo viwanja ndio vilikuwa vinatolewa na watu kuanza ujenzi wa nyumba.
“Unafnyaje huko?” nikamuuliza baada ya kukosa la kumwambia.
“Ndiko ninakoishi”
“Nataka nije nikuone”
“Kwa ajili gani?”
“Tujuane tu”
“Kwa lini?”
“Kwa leo”
“Haitakuwa rahisi”
“Kwanini…”
Alikuwa ameshakata simu. Nikampigia tena lakini simu yake ikawa haipatikani. Nikaachana naye.
Jioni ya siku ya pili yake nikampigia tena. Simu yake ikawa inaita. Iliita kwa muda mrefu kasha ikapokelewa.
“Hallow!” Sauti yake laini ikasikika kwenye simu.
“Hujambo?” nikamuuliza.
“Sijambo”
“Habari ya tangu jana?”
“Ahaa… wewe ndio yule jamaa wa jana?”
“Ndiye mimi. Nimekumiss…”
“Kumbe wewe uko Tanga?”
ITAENDELEA  ili usipitwe hakikisha una shuka hadi sehemu ya followers kisha bofya sehemu hiyo

No comments

Theme images by konradlew. Powered by Blogger.