Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi 03

Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi 03


Tulikwenda kwenye mlango, Erick
akabisha mlango huo na punde tu
ukafunguliwa na msichana
aliyeonekana kama msomali.
Alikuwa mweupe na mwembamba
kiasi. Alipotuona alishituka na
kutuambia.
“Assalam alaykum”
Erick ambaye alikuwa amezoea
salaam hizo za kipwani ndiye
aliyemuitikia.
Nilidhani afande Erick angemuulizia
mwenye nyumba lakinihakufanya
hivyo, alitoa kitambulisho chake
akamuonesha yule msichana.
“Sisi ni polisi wa upelelezi kutoka
jeshi la polisi. Tumepata taarifa
kuwa humu ndani mnauza
madawa ya kulevya. Je ni kweli?”
Msichana aliposikia hivyo
alishituka.
“Si kweli” akajibu kwa kubabaika.
“Sawa. Sasa kilichotuleta hapa ni
kufanya upekuzi katika nyumba
hii”
“Ngoja nimuite mama”
Aliposema hivyo mwanamke
mmoja mzee akatokea nyuma
yake.
“Mnataka nini?” akatuuliza. Kidogo
alikuwa na lafidhi ya kiarabu.
SASA ENDELEA
Erick akamueleza kazi yetu na
kusudio lililotuleta kwenye
nyumba ile.
“Karibuni” mwanamke huyo
akatuambia.
Tukaingia ndani.
“Sisi hatufanyi biashara hiyo na
wala hatuijui. Sisi tunauza
mapambo ya wanawake tu”
Mwanamke huyo akatuambia
tulipokuwa ndani.
“Tumepata taarifa ya kuaminika
kuwa mnauza madawa ya kulevya,
kwa hiyo tunataka tufanye upekuzi
humu ndani” Erick akamwambia.
“Sawa. Fanyeni upekuzi wenu. Sisi
hatuwezi kuwazuia. Lakini kuingilia
faragha ya mtu si jambo zuri”
Tukaanza kufanya upekuzi wetu
bila kuwepo na shahidi wala
mwenyekiti wa mtaa. Tulianza
kupekua kwenye lile duka. Kisha
tukaendelea kwenye vyumba
vingine. Tulipoingia chumbani kwa
yule binti nilimuona Erick akitoa
kitu kwa siri mfukoni mwake kisha
akainama chini ya kitanda.
Aliponyanyuka alionyesha kile kitu
alichokitoa mfukoni mwake,
akauliza.
“Hiki ni nini?”
Erick alikuwa ameshika kete tatu za
madawa ya kulevya. Alikuwa
amemtumbulia macho yule
mwanamke.
“Nimekuuliza hiki nini?”
“Sisi tutajuaje? Kitu umekishika
wewe halafu unatuuliza sisi,
hatuwezi kujua” Yule mwanamke
alimjibu.
Erick alijifanya ananusa zile kete
kisha akaniambia.
“Ni kete za madawa ya kulevya.
Ndiyo haya tuliyokuwa
tunayatafuta”
“Zinaonekana kuwa ni kete kweli”
nikamkubalia.
“Hebu nusa”
Alinisogezea kete hizo kwenye pua
yangu. Nikazinusa.
“Ni kokeni yenyewe!” nikasema na
kuongeza. “Kweli sasa nimeamini
hawa watu wanafanya biashara ya
madawa ya kulevya”
Ilikuwa kama nimemchochea Erick.
Akamtazama yule mwanamke kwa
macho makali.
“Mama ulikuwa unakataa?
Tumekuta kete hizi za madawa ya
kulevya chini ya kitanda cha binti
yako!”
Mwanamke huyo na binti yake
walibaki kushangaa.
“Kete za madawa ya kulevya ndio
nini?” Mwanamke huyo akauliza.
Binti yake akabetua mabega.
“Sijui”
“Bila shaka kutakuwa na kete
nyingi humu ndani. Ngoja
tuendelee kupekua” Erick akasema.
Tuliingia katika chumba kingine
ambacho kilikuwa ni cha yule
mwanamke. Katika kupekua
tulikuta kisanduku cha shaba
kilichowekwa ndani ya kabati.
Tulipokifungua tulikuta kimejaa
mapambo ya dhahabu.
“Mmepata wapi dhahabu hii?” Erick
akawauliza.

Recommend 👇
 Kwa Habari
           Ajira
           Motivation
Bofya link iliyopo hapo chini

https://t.me/alvinhabari

Pia hakikisha una join hiyo telegram  channel


“Sisi tunafanya biashara ya
dhahabu” Yule binti akamjibu.
“Hii pia itakuwa mali iliyopatikana
kwa njia ya haramu!”
“Hapana, tunanunua kihalali”
Msichana ndiye aliyekuwa akisema.
Yule mwanamke alionekana kama
amepandwa na presha.
“Mtakwenda kujieleza vizuri polisi”
“Mnataka kutupeleka polisi?” Yule
mwanamke aliyekuwa kimya sasa
aligutuka na kuuliza.
“Kama hamtaki kwenda polisi
tunaweza kuzungumza na
kuyamaliza hapa hapa. Hii kesi ni
kubwa sana”
“Huyu mama pia hataweza
kifungo” Na mimi nikasisitiza.
“Sasa mnataka tuzungumze nini?”
Mwanamke huyo akatuuliza.
“Hujui? Utatupa kiasi gani ili
tukuachie?”
“Mimi siwezi kutoa rushwa kwa
sababu hatujafanya kosa lolote”
Maneno yale yalimuudhi Erick.
Nikaona uso wake umebadilika.
“Hamjafanya kosa lolote, si ndio…?”
akasema huku akitoa simu. Hapo
hapo akawapigia polisi wenzetu
waliokuwa kituoni. Aliwaeleza
kilichotokea na kwamba alikuwa
anahitaji gari.
Je nini kitaendelea? Usikose
kuendelea na hadithi hii hapo
kesho.

No comments

Theme images by konradlew. Powered by Blogger.