MPENZI WANGU HAKUWA BINADAMU BALI KIUMBE ASIE WAKAWAIDA

 KARIBU KWENYE STORY YA MAISHA YANGU YA MAHUSIANO  AMBAYO SIWEZI KUSAHAU NILIVYO PENDA KIUMBE WA AJABU



Nikiwa kwenye early 20's nilidate na huyu manzi she was beutiful though was a bit taller kunizidi kidogo, hiyo kipindi naanza chuo ye alikua na ajira ya serikali kwenye sekta ya afya, hiyo moment mi nilikua chuo, tulikua mikoa karib  weekend nyingi tulispend pamoja it was funny

Niseme nilikua huru nae sana kuliko kawaida the same she was kwang yan ilikua hata zile night mfano anahitaj umkamue havungi yan atauliza kwahiyo leo vipi au walaah hapo ni kupiga spana tu had maji yakauke kwenye miili yetu, she was always happy with Me the same I was kwake

 Hasa siku zote huwa naamin mtu akiwa na hasira msikilize kwa makin sana manake ataongea hata yale ambayo alipokua kawaida alishindwa kuyatoa kifuani kwake, kuna siku tulikua tumetoka kula somewhere dizain kuna kitu tulipishana so dizain kama kanuna flan nikaona poa tu yataisha

Tukiwa tunatembea kuna rafiki yangu wa kike mwingine She was very funny untill this day yupo charming sana akawa kanipigia simu ile nimepokea nikawa ile normal nacheka tunastorisha kumbe mwenzangu akapata moto ile mbaya tulipofika home akamaind ile hatar akatapika nyongo yote 😳

Bas one of the thing alinambia usitake nikuoneshe upande wangu wa pili upoje akakomaa yule ni pia ni chombo ya fundi mjuba nikagoma katakata akanambia kitu kimoja yule sio mwanamke wako ndio lakini anakutaka its just a matter of time tu utaanza kutoka nae sikuyapa nafasi hayo but

 Kuna kitu aliropoka ambayo ilinifanya nipigwe ganzi ghafla alinambia usione mtu anapiga issue flan ukawa fooled kuna meng nyuma ya pazia imagine that beutiful girl alikua nje ya ile job yake kuke sekta ya afya alikua ana pharmacy somewhere lakin mwenyewe anasema ilikua geresha tu


But the real deal alikua anafanya ilikua ishu za unga 😭😭😭, hapa mapigo ya moyo yalivurugika na kuna kile kijasho cha kwapa kilitoka nikaona nisha mess up tayari nikajisemea moyoni huyu natakiwa nimpige chini chap asije niingiza matatizoni kumbe najiongopea tu sio rahis hivyo

Mapenzi yana nguvu kuna watu wanasema mapenzi yana nguvu kama mauti wanaweza kuwa wapo karibu na ukweli, ule mshtuko wang hata yeye aliuna dhahiri naona akajua ashavujisha siri za kambi tayari nadhan walio kwenye mahusiano wanajua ugomvi huwa unaishaje yan aisee ile siku kitu

Nilifanywa had nikatia akili nilipewa ile kampa tena tena had nikahis mimi ndio nafanywa sio yeye tena kiufup nilikua over dozed nikajua hapa ni mambo ya kuombana msamaha in adult way wakat mi nawaza huyu wiki haiishi napiga chini baada ya kaz kazi tumelala tunastorisha akasema

Unajua hiz kazi za kawaida hadi utoboe maisha sio leo ndo mana mimi napiga hizi dili, akanielekeza namna zinavyofanyika namna mzigo unavyosafirishwa kwa mbinu tofaut na namna unavyosambazwa na kuwa ile business once ukiingia No kutoka ukitaka kutoka they kill you once for all 😭

Saa hiyo naambiwa hayo makitu akili haisomi nikajitutumua kumuuliza huon kama una risk sana ukidakwa inakuwaje, bora hata nisingeuliza hili swali nilijuta majibu niliyopewa yan, akanambia unadhan mimi ni wa kawaida, mi mwenyewe nimejizatiti nipo full siingiliki kirahis but how

Akanambia ndumba zinahusika 😭nikaona hizi nyege zimenileta kwa huyu mwanamke ntajinasuaje sasa na ndumba tena mambo gan haya sasa😢, akaniambia unakumbuka kile kipindi umeumwa hii itokea kama wiki 3 hv nyuma nikamjib yes akasema sababu unaijua nikamwambia hapana akasema ni yeye

Nikamuuliza sabab ni yeye kivip akanambia uliumwa kwa sabab uliziona kucha zang hukupaswa kuziona had kuna means flan ifanyike nikazid kupagawa na kiukwel all the time alikua kucha zake anazipaka rangi nikakumbuka kwel kipindi nimeona kucha zake hakua kapaka rangi yoyote ndo homa

Ikanipiga kwenda hospital nikaambiwa nothing wrong nipate muda wa kutosha tu wa kupumzika hapa akil ikawa kama imepigwa shoti, haya yanatokea muda mfupi baada ya ule mtanange tupo naked ndan ya shuka yan kanilalia kwa kifua na kwangu haikua romantic talk ila ilioniogopesha mno 😔

 Akaendelea unajua mimi yule unayemfaham sio baba yangu japo ye anajua mi ni mwanae nikauliza how could this be possible ndo akaniambia kitu cha kushangaza zaid akanambia kama ushawah sikia nakwambia naenda kigambon kwa mshua bas kule ndo nyumban kwa baba yangu halis nikahis labda

 Ndo zile mambo mtoto ana baba ake wa nje mama alichepuka baadae anakuja kumchana mtoto baba ako halis ni flan bt I was wrong completely that girl was half human being and half sjui niiteje nadhan mmenielewa so ilifikia point nikawa namuogopa kuliko kawaida manake alikua anawaweza

Anaweza kuniambia issues zang ambazo hata sijawah kumwambia mfano kuna manz nilikua nae akawa ananiambia una mwanamke mwingine zaid yang kila mara akileta hii mada I end up denying but akawa ananiambia we bisha lakini naona kivuli cha mwanamke kwako 😭,  nikawa naona I am fucked

 But always alikua ananisistiza hawez nidhuru something I couldn't believe hata kidogo nilikua najiona mbuzi wa kafara tayar anytime ntatembezwa viwanja nikawasabah kuzimu, nikawa nakonda bila sabab na kumuacha sina ujasiri kabisa, nikawa najipa ujasiri tu Muumba ataniokoa japo

 But always alikua ananisistiza hawez nidhuru something I couldn't believe hata kidogo nilikua najiona mbuzi wa kafara tayar anytime ntatembezwa viwanja nikawasabah kuzimu, nikawa nakonda bila sabab na kumuacha sina ujasiri kabisa, nikawa najipa ujasiri tu Muumba ataniokoa japo

 Sikuwa namuomba hata baadae akawa romantic had kupitiliza kidogo ikawa kama inaniaminisha kuwa this shall pass but how sikuwah kujua, siku moja nakumbuka tumewah kwenda kwao nikaonana na baadhi ya members wa familia yake akanambia same story kuwa wale wamezaliwa mama moja lakini

Baba ye anae wake tofauti na wao lakin hakuna anayejua only Her, nikajisemea hapa nilivagaa mkenge kabisa sijui hata nilifikaje kwake but naamin kila kitu kinatokea kwa sabab maishani nothing happen by accident, katika umri wake wa miaka 23 tu alikua tayr anasukuma  VX Limited

 Gari ambayo kwa kipindi kile ilikua ni anasa na iliagizwa toka Joberg, sema hakuwa mtu wa show off so ilikua ni nadra utamkuta anazungumzia mali anazomilik au kumkuta yupo obsessed na gari alikua anatembelea mara chache  nikajisemea mimi level zangu ni za akina mwajuma sio huyu

 Wakati mwingine nikikumbuka huwa nashindwa kuelewa niljinasua vip pale lakin kuna siku ambayo nadhan ndio ilitengeneza mwanzo wa mimi na yeye kuachana tulikua kivukon akaniomba nimpelekee mzigo dada ake magomen usalama then tutachekiana kwa simu alikua anaenda kwenye dili za unga

Ile ndio ilikua siku pia ambayo nilijua kabal za vibaka zinafananaje, nimepeleka mzigo frsh ni yale maeneo ilipo ile shule ya baptist wenyej wanapajua kuna kichochoro kinaingia kibarabara cha mtaa wakat wa kurud road wahuni wakanitaitisha loba moja heavy nikahis roho inaacha mwil

Wakatembea na laptop, simu na chenji zote nilizokua nazo hiyo ni saa 4 kasoro usiku, nikasema bora uhi wameniachia mali zinatafutwa, nikapiga hesab wap niende nilikua na washkaji magomen mapipa ukishuka kituoni unapita bondeni hotel pale ule mtaa wa nyuma then unashuka chin kule

 Lakini it was too risk manake kuna vibaka hatar ndo wangenimaliza kabisa, option ya pili niende Kimara barut but mhusika ndo tumeachama kigambon kaenda kwenye mishe za hatar nikaua lile wazo na kumbuka saa hoyo sina hata 100 kwahiyo natakiwa nitembee kwa mguu, nikaona niende UDSM

Kutoka pale magomeni usalama nikaanza kutembea kwa mguu pita kituo hadi kituo nafata barabara hadi nafika mlimani pale nikaenda kulala kwa jamaa zangu Hall 6 walikua wanasoma pale hiyo mida mibovu saa 6 usiku huko, sikusema chochote asubuh next day ndo nikampa story mshikaji kuwa

Nini kilinisibu had kuwa katika hali ile hapo ndo nikaomba simu nikamchel yule manzi akanabia panda gar utanikuta dukani kimara nikachukua nauli kwa mwana nikasepa, kufika kule napewa pole na nini manake ni kama na yeye alichangia kwa sehem flan kutokana na miscommunication

 Mida flan ya jion kwemye saa 10 hiv akatoka akaenda sehem akaniambia anarud in an Hour, hakwenda mbali ni around hapo hapo kwel later anarud naona mtu anavuja maji kalowa mwil mzima ila nguo zake kavu nikamuuliza vip ulienda kuoga akanijib No nilienda nyumban kwa baba Kigamboni😭


 Daah ule mwaka aisee nilipitia Mengi kama mawazo hayakuniua na stress bas haviwez kuniua tena aisee,  akaniambia kuna masharti alipewa ila ye akawa anakiuka mojawapo ni kuwa asitumie kilevi chochote so alienda kutumikia adhab alipewa tukaongea mengi hut akawa anataka anilipe vitu

 Nilivyoibiwa mimi nikamgomea nikamwambia hahusiki navyo katika upotevu wake kwa namna yoyote ile awe na aman, then wiki iloyofuation nikaondoka ule mkoa baada ya hapo nikaanza kupunguza mawasiliano nae taratibu had ye mwenyewe akajua kuwa sipo comfortable for issues kwake

Na kweli kuna mazingira yalikua yananipa ugumu imagine amedakwa na mwera kwenye mishe zao huko kawekwa nyuma ya nondo unaachaje kwenda kumchek usipoenda inaweza kutafsirika huna mapenzi nae na ukienda unaweza kuwa suspect na wewe ukaunganishwa kwenye mambo ambayo hata hayakuhusu

Pamoja na mambo mengine yote yaliyotokea ambayo siwez kuyaandika hapa yote but kwake kuna mengi nilipata kuyajua kuhusiana na ulimwengu wa giza jinsi unavyo operate na yanayofanyika huko, mfano aliwah kuniambia ukiwa kariakoo mchana wakati wa jua kali kuna watu weng huwa sio watu

 Alinambia wewe unaweza kuona ni watu lakini huwa sio watu na kuna namna ya kuwatambua kuwa yule ni mtu na yule sio ni kiumbe kingine  na akanambia hiyo mida usipende kukaa chini ya miti mikubwa ya asili hasa ukanda wa pwani kuanzia Tanga, Dar, Z'bar, Moro, Lindi na Mtwara

 Kuna story imewahi kuandikwa sikumbuki kwenye gazeti gani lakini ilikua inasema karibu robo au nusu ya population iliyopo dar sio binaadam ni majini...sijui kuhusu hizo figures but kuna ukwel kuwa sehem flan ya population sio watu kwa mujib wake na ilikua hata tukiwa misele kitaa

Alikua ananiambia kabisa unamuona yule pale sio mtu, ye alikua anawajua kwa sabab nadhan ya the way alivyozaliwa kama nilivyosema juu kule, kupitia yeye nilijifunza pia kuwa kuna baraka nyingi katika kusaidia wasiojiweza mfano yatima, maskin, wajane na wazee kuna kauli alikua

Anaitaja mara nyingi akawa anasema ukifanya hivyo kwa hulka yake yeye alivyo mambo yako mengi unafanikiwa ila mbinguni huwezi kwenda sijui kwanini alikua ananiambia hawez kwenda mbinguni sikuwa na ujasiri wa kumuuliza hili, niliishia kupiga kimya tu manake ningejitaftia presha tu

 Nakumbuka kuna siju amewah kuniambia kitu cha ajab sana kuhusu mimi alinambia kimi sipo kokote, kwa shetani sipo wala kwa Mungu sipo 😭😭😭, So kama sipo huko kote nipo wap sikuwah kuwa na majib na ile kauli lakini ule ulikua mwanzo wa kunofanya nianze kujiweka karibu na Muumba

 Baadae tuliachana for good manake mapenzi yalikuja kupoa mno kama mkojo wa ngedere yani, mara ya mwisho alintafuta nikiwa bado nna account facebook akanijulia hali lakini sikua comfortable kabida kuchat nae na hiyo ilifanya ile account niifutilie mbali na sijawah fungua nyingine

 Najua wengi wanataka kujua pengine yuko wapi nowadays anyway sina habari zake ila najua aliolewa na anaishi jijini dar na alikua mtoto mmoja had last time nikiwa na habari zake, haya yote nimeyaandika hapa nilikutana nayo nikiwa na umri wa miaka 21 tu it was Scary 😢😢

Mwisho.
Credit:Masha
Writer🖋️:iqram
Publisher:Alvin



NAKUSHUKURU SANA KWA KUTEMBELEA BLOG HII KARIBU TENA MAMBO MAZURI YANAKUJA ACHA COMMENT YAKO APO CHINI KUHUSIANA NA BLOG HII KIPI KIPO VIZURI AU KIPI HAKIJAKAA POA  PIA NAKUOMBA SHARE KWENYE SOCIAL MEDIA ULIZOPO let's support ourselves
Link
https://alvinhabari.blogspot.com

No comments

Theme images by konradlew. Powered by Blogger.